Ijapo safari iwe na ugumu
Utanishika mkono
Ijapo adui aje kwa vishindo
Bado wewe uko nami
Iwapo safari iwe na huzuni
Utayapanguza machozi
Ijapo adui aje kwa vishindo
Bado wewe uko nami
Chorus
Utayarejesha maono yangu
Miaka yote iliyoliwa na nzige
Nimeona wema wako
Na nguvu zako maishani mwangu
Iwapo safari iwe na giza
Utaangaza njia zangu
Ijapo adui aje kwa vishindo
Bado wewe uko nami
Iwapo safari iwe na ukame
Wewe ni maji ya uzima
Ijapo adui aje kwa vishindo
Bado wewe uko nami
Chorus
Utayarejesha maono yangu
Miaka yote iliyoliwa na nzige
Nimeona wema wako
Na nguvu zako maishani mwangu
Refrain
Akisema ndio akuna wa kupinga
Nitasimama kwa agano lake
Nimeona aa wema wako
Na nguvu zako maishani mwangu
Akifungua mlango hakuna atakaye funga
Amesema amesema, Hakuna wa kupinga
Nimeona aa wema wako
Na nguvu zako maishani mwangu
Akikubariki hakuna wakupinga
Simama leo kwa hilo neno
Nimeona aa wema wako
Na nguvu zako maishani mwangu
Akikuponya wewe umepona
Simama leo kwa ahadi zake
Nimeona aa wema wako
Na nguvu zako maishani mwangu
Chorus
Utayarejesha maono yangu
Miaka yote iliyoliwa na nzige
Nimeona aa wema wako
Na nguvu zako maishani mwangu
Comments
Post a Comment